WATENDAJI UYUI WAAGIZWA KUFIKISHA ASILIMIA 100 YA MAPATO YA NDANI IFIKAPO DESEMBA

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui wakiimba wimbo wa Taifa kabla Baraza lao halijaanza Septemba 6, 2021.

Na Tiganya Vincent, Uyui

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui limetoa miezi minne kwa kwa Watendaji wanaohusika na ukusanyaji mapato kuhakikisha wamefisha asilimia 100 ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ifikapo Desemba mwaka huu.

Kauli hiyo imetolelewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Said Ntahondi kwa niaba ya Madiwani wenzake na wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani.

Alisema miezi ya kukusanya mapato kupitia vyanzo vya ndani imebaki mine ni vema watendaji wakahakikisha wanashirikiana na  Madiwani ili watumie miezi iliyobaki kufikia malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi bilioni 2.4.

Ntahondi alisema Desemba shughuli za kilimo zikianza kama watakuwa hawajaifikia lengo itakuwa vigumu kukusanya kiasi walichojipangia.

Aliwataka Madiwani kuhakikisha wanawasimamia kwa karibu Watendaji wa vijiji ili waweze kuonyesha mpango wao wa ukusanyaji wa mapato na wautekeleze kwa vitendo.

Mkuu wa Wilaya ya Uyui Kisare Makori alisema  wakusanyaji wa mapato wanatakiwa kuwa waadirifu kwa kuhakikisha fedha zote zinakusanywa zinakwenda sehemu husika.

“Ndugu zangu Madiwani hakikishe kila senti ya Serikali inayokusanywa inapelekwa katika shughuli za maendeleo ya wananchi…pia hakikishe mnaziba mapengo ya upotevu wa mapato ya Serikali”alisitiza.


Comments

Popular posts from this blog