ĎKT. NDUMBARO AZITAKA NCHI ZA AFRIKA KUWA NA KAULI MOJA KUHUSU UWINDAJI WA KITALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (kuli) akizungumza na  Waziri wa Utalii wa Zimbabwe kuhusiana na kuwa na bei ya pamoja ya uwindaji wa kitalii katika nchi wanachama wa SADC katika kikao pembeni katika  Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL  nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Na Mwandishi Wetu, Cape Verde
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka nchi za Afrika kuwa na kauli moja kuhusu taratibu na bei  za wanyamapori  katika biashara uwindaji wa kiutalii
Ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti katika vikao  ana  kwa ana na baadhi ya  mawaziri wa Utalii wa nchi za Afrika katika Mkutano wa 64 wa  Kimataifa wa Utalii uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Kimataifa la Utalii Duniani  (INWTO) unaofanyika kwa muda wa siku nne nchini Cape Verde.
Amesema bei za wanyama wanaoruhusiwa kuwindwa pamoja na vitalu vya uwindaji wa Wanyamapori zimekuwa zikitofautiana sana kati ya nchi na hali hali hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwa shughuli uhifadhi barani Afrika.
Akizungumza katika vikao hivyo vya ana kwa ana na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe.Mhe.Ngobhithize Ndlovu  amezitaka nchi hizo kuwa kitu kimoja katika kuamua na kupanga bei za uwindaji wa Kitalii.
Amesema kutokana na kutofautiana kwa bei na baadhi  ya kanuni na taratibu hizo  Wawindaji wa kiitalii wamekuwa wakitumia mwanya huo  kuzikandamiza nchi za Kiafrika kwa kupanga bei wanazotaka wao huku wakidai kuwa bei hizo cha chini zimekuwa katika nchi nyingine pia.
Amesema Wawindaji hao wamekuwa wakipanga  bei za uwindaji wa kiutalii na sio nchi husika huku wakidai kuwa kama bei hiyo haitawezekana basi watakwenda katika nchi nyingine ambayo utalii wake uwindaji ni bei ya chini zaidi
” Utofauti wetu huu umekuwa ukitukandamiza kama nchi kwani tulitakiwa sisi ndo tupange bei lakini kutokana na kutokuwa na umoja bei za wanyama  zimekuwa zimekuwa zikiamuliwa na wao  hili lazima tulikatae kwa kuungana kwa pamoja ” alisisitiza Dkt.Ndumbaro
Kufuatia hali hiyo, Dkt.Ndumbaro amezitaka nchi zote zinazoendesha utalii wa uwindaji zifanye mkutano kwa nji ya mtandao ili kujadili mustakabali wa biashara hiyo na kisha  zitoke na kauli moja ili kuwathibiti wawindaji wa kitalii kwa ajili ya maslahi mapana ya uhifadhi barani Afrika.
Amezitaja baadhi ya nchi wanachama wa SADC zinazofanya vizuri katika uwindaji wa kitalii kuwa ni Botswana, Zimbabwe pamoja, Zambia na Afrika ya Kusini 
Katika hatua nyingine , Dkt.Ndumbaro ametoa ahadi kwa  nchi ya Zimbabwe  kama itakuwa  tayari ipewe mafunzo ya kuendesha biashara ya uwindaji wa kiutalii kwa mfumo wa kidigitali ambao utasaidia kuongeza mapato maradufu
Amesema tangu kuanzisha kwa mfumo huo nchini Tanzania umeleta manufaa makubwa kwa nchi  ambapo Wawindaji wa kitalii ili kuweza kupata vitalu vya uwindaji wamekuwa wakilazika kushiriki katika mnada wa kimtandao.
Naye, Waziri waUtalii wa ZimbabweMhe.Ngobhitithize Ndlovu amesema nchi za kiafrika lazima ziungane katika suala hilo kwani katika nchi ya Zimbabwe Wawindaji hao pia wamekuwa wakipanga bei huku wakidai kama hiyo bei haitawezekana watakwenda Tanzania ambako bei vitalu vya uwindaji ipo chini zaidi
Amesisitiza kuwa shughuli za uhifadhi zimekuwa aghali sana huku biashara hiyo ya uwindaji wa kiutalii ukibaki pale pale kutokana na kutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine
Naye, Kamishna Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mabula Misungwi amesema umoja huo wa nchi za Kiafrika katika biashara ya vitalu vya uwindaji italiingizia taifa fedha nyingi za kigeni sio kwa Tanzania pekee bali kwa Afrika nzima
” Biashara hiyo imekuwa na ushindani baina yetu bila kujuana kufuatia kila nchi kupanga bei zake kulingana na matakwa ya wadau hao huku shughuli za uhifadhi zikiwa juu zaidi” amesisitiza Kamishna Mabula.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe   mara baada ya kikao cha kujadili uwindaji wa kitalii pembeni mwa Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL  nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.Kulia ni Balozi wa Paris Ufaransa Mhe.Samweli Shekindo pamoja Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii ya Zimbabwe Dnomal dinamo

 
Kamishna Uhifadhi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Prof. Dos Santos Silayo (wa kwanza kushoto) akiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Philip Chitaunga  wakishiriki katika kikao cha ana kwa ana kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro (juu kulia) akizungumza na Waziri wa Utalii wa Zimbabwe kuhusiana na kuwa na bei ya pamoja ya uwindaji wa kitalii katika nchi wanachama wa SADC katika kikao pembeni katika  Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL  nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Afisa Utalii kutoka Bodi ya Taifa yaUtalii ( TTB) Naomi Mbilinyi ( wa pili kulia) akiwa akifuatilia mada ya kutumia mitandao ya kijamii katika kutangaza vivutio vya utalii katika Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL  nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na Waziri wa Utalii wa Gambia, Mhe. Hamat Bah  mara baada ya  Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL  nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na Waziri wa Utalii wa Nigeria, Alhaji Mohammed katika mara baada ya  Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL  nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro akizungumza na jambo na Waziri wa Utalii wa Kenya , Mhe. Najib Balala katika mara baada ya  Mkutano wa  Kimataifa wa  64 wa Utalii Kanda ya Afrika  ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Utalii (UNWTO) unaoendelea  kufanyika katika kisiwa cha SAL nchini Cape Verde, Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri wa Utalii 30 lengo likiwa ni kujadili mustakabali wa utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla ambapo wamekubaliana kushirikiana katika kutangza vivutio vya utalii kwa pamoja kama Bara la Afrika.

Comments

Popular posts from this blog